Ronaldo Amesema Soka La Hispania Bila Shaka Ni Bora Katika Historia Na Itakuwa Vizuri Kwa Coutinho Kuthubutu Kucheza Na Wachezaji Bora Duniani
Mshindi wa Kombe la Dunia Ronaldo amekiri kuwa angependa kumuona kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho akicheza Real Madrid.
Nyota huyo, 24, amekuwa akifanya vizuri tangu alipotua Anfield akitokea Inter Milan mnamo 2013, tetesi zikipamba moto kuwa Barcelona au Paris Saint-Germain zinaitaka huduma yake.
Hata hivyo, Ronaldo anataka Coutinho ambaye ana mkataba Liverpool hadi 2020 - akihama meli na kujaribu maisha mengine na wachezaji bora wa La Liga wanaokipiga Real Madrid.
"Ningependa kumwona Coutinho Real Madrid," aliiambia redio ya Hispania Onda Cero. "Soka la Hispania, bila shaka, ni bora katika historia. Wamekuwa wakinunua wachezaji bora na kuzalisha soka lenye mvuto zaidi."
Ronaldo amecheza miaka mitano Bernabeu, akifunga mara 104 katika mechi 177 Real Madrid na kuiwezesha timu yake kutwaa mataji mawili Hispania.
Comments
Post a Comment