Ndege Ya Abiria Ya Air France Yapata Shida Kwa Kuharibikiwa Na Injini Ikiwa Angani
Ndege hiyo superjumbo ilikuwa njiani kuelekea Los Angeles- Marekani kutoka mji mkuu wa Ufaransa- Paris, ikiwa na zaidi ya abiria 500.
Iliamua kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Goose Bay, mashariki mwa Canada.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika kisa hicho, lakini abiria walisalia ndegeni kwa saa kadhaa, baada ya ndege hiyo ya abiria kutua.
Wakati wa kisa hicho, ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 496 na wafanyikazi 24. Hayo ni kwa mjibu wa msemaji wa Air France spokesperson, aliyezungumza na shirika la habari la AFP.source @bbcswahili.com
![]() |
| BESTHANDSDAY WISHES YOU OUR GRATEFUL FOLLOWER HAPPY NEW MONTH |


Comments
Post a Comment