HIZI NDIO HABARI KUBWA KUBWA KUBWA 5 ZILIZOTOKEA WIKI HII

Kila Jumapili Usikose Kuangalia Your Best Five News Hapa Hapa Kwenye Best Blog In Globe 

Best 001 :)

Wiki  ilijaa masikitiko makubwa hususani kwa wapenzi wa mchezo wa mpira duniani kote baada ya timu Chapecoense kupata ajari ya ndege wakiwa wanaokwenda kucheza fainali na timu ya Columbia, na ivyo ajari ikatokea iliyosababihswa na kuisha mafuta kwa ndege iyo. Watu 71 walipoteza maisha, mchezaji mmoja tu ndio aliyenusurika katika ajari iyo na inasemekana anaweza kurejea uwanjani kwa muda ujao, Pia kwa sasa mashabiki wa Chape wanampigia upatu mchezaji wa Brazil gwiji Ronaldhino kujiunga na timu iyo kama hisani yake kwa kile kilichotokea kwao.

Best 002 :)


Huyu mzee bwana hakosi neno kila akifika leo, Trump aliyeshinda uchaugzi wa Marekani kwa kura zote za msingi mnamo Novemba 8, alisema kwa vyombo vya habari kwamba pamoja na ushindi wake kua wa kishindo bado kuna mamilioni ya wapiga kura waliopiga ki wizi wizi na kufanikiwa kuibuka mshindi mbele yao, sasa uyu mzee hapo kashinda na anasema kaibiwa je angeshindwa inekuaje? Pia amekiri kuachana na maswala ya biashara na kuweka mkazo kwenye kuifanya America Great Again.

Best 003 :) 


Umoja wa nchi zinazozalisha mafuta duniani wakiongozwa na Saudi Arabia OPEC ndani ya ili juma walikutana mjini Vienna na kuweka mkakati wa kupunguza uzalishaji wa mafuta na ivyo kupelekea bei ya mafuta kupanda bei kwa asilimia 8, hata ivyo Tanzania kupitia wizara ya nishati imetoa tamko kwamba hatari hizo za bei zitaanza rasmi mwezi wa 4 mwakani, wenye vyombo vya usafiri mjipaneg.....

Best 004 :)


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli inasimamia nidhamu ya kazi na heshima kwa wananchi, hivyo kutaka kila mmoja atimize wajibu wake. Aidha, imeonya kuwa fedha za miradi ya serikali ni za moto hivyo ziachwe sifanye shughuli zilizokusudiwa, kwani zikichezewa lazima zitaunguza mtu au watu. Aliyasema hayo jana jioni alipozungumza na wananchi wa Jiji la Arusha waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.....more on habarileo.co.tz

Best 005 :)

Rapa kanyewest ametoka hospitali baada ya kupata ugonjwa wa uchizi alivokua anafanywa show juma moja lililopita. Rapa uyo maarufu na nyimbo zake kali kama Stronger, good life alijikuta akiongea maneno ya kashfa kwa swahiba wake wa muda mrefu Jay z, Beyonce na Drake. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini marekani, rapa uyo ameingiza watu hasara kubwa , waandaji, mashabiki na wahudumu waliokua wamejiandaa kushirikiana nae katika ziara yake iliyoarishwa baada ya kupelekwa hospitali.

# Dribble da mania

Comments