SIMBA YAPATA JEMBE,AZAM YAMSAJILI HUYU..

Simba Yapata Mbadala Wa Mkude Simba Anayesuasua Kusaini Mkatba Mpya,Wakati Azam Ipo Mbioni Kumsajili Joseph Mahundi



Simba imepania kumaliza jeuri ya Nahodha wake Jonas Mkude, anayedengua kusaini mkataba mpya baada ya kumleta nchini kiungo James Kotei raia wa Ghana anayecheza nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe, amesema, kama wataafikiana na kocha kumkubali watampa mchezaji huyo mkataba wa miaka miwili na kuanza kazi mara moja.

“Tunataka kumaliza zoezi hili kabla ya dirisha la usajili kufungwa, tayari mchezaji tumempeleka Morogoro ilipo timu na kama kocha ataridhia kiwango chake basi tutaingia naye mkataba,” amesema Hans Poppe.

AZAM FC
Azam  FC inatarajia kumtangaza winga wa Mbeya City Joseph Mahundi, kama mchezaji wao atakayeitumikia timu hiyo kwenye mzunguko wa pili baada ya kukaribia kukamilisha taratibu za usajili wake.

Mtendaji mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amesema, mazungumzo yaliyopo kwa sasa kati yao na Mbeya City, ni kiasi cha pesa za usajili, na baada ya zoezi hilo kukamilika tayari nyota huyo atakuwa mali yao.

“Tunashukuru ushirikiano mzuri tunaoupata kutoka kwa wenzetu wa Mbeya City, tunaamini zoezi hili halitachukua muda mrefu kwa sababu tumedhamiria kumchukua mchezaji huyu kutokana na kuridhishwa na kiwango chake,” amesema Kawemba.

Comments