Kocha Wa Arsenal Arsene Wenger Amesema Haogopi Kupangiwa Na Real Madrid Hata Bayern Munich Kwani Timu Yake Kwa Sasa Ipo Imara
Washika Mtutu hao walitinga hatua ya mtoano wa michuano hiyo kwa kumaliza kinara wa Kundi A baada ya ushindi wa nguvu wa jumla ya goli 6-1 dhidi ya Basel Jumatano usiku.
Arsenal walisaidiwa na Ludogorets Razgrad, ambao waliizuia Paris Saint-Germain kwa sare ya 2-2, lakini pia wanaweza kukutana na miamba wa Kihispania Real Madrid katika hatua hiyo ya 16-Bora.
Vijana wa Zinedine Zidane walikuwa wakiongoza kundi lao baada ya kupata mabao 2-0 katika mechi yao dhidi ya Borussia Dortmund, lakini wapinzani wao wa Ujerumani walipambana vikali na kuishusha Real Madrid hadi nafasi ya pili.
“Ukitazama timu ambazo tunaweza kukutana nazo, nyingine zinaonekana kuwa na hadhi kubwa, ngumu zaidi, nawe ungependa kunisikia nikisema ‘Siitaki timu hii au timu ile’ lakini hilo litatuweka katika nafasi ya udhaifu ikiwa itatokea hivyo,” Wenger aliwaambia waandishi kwenye mkutano wa wanahabari wa Alhamisi.
“Tunaweza kukutana na Real Madrid, miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa kushinda michuano hii, hata tukicheza dhidi yao tunayo nafasi ya kufuzu. Changamoto nyingine kwetu, hatujawahi kufuzu miaka sita iliyopita kucheza robo fainali. Hiyo itakuwa changamoto kubwa kwa kundi langu na tutaifurahia.”
Wakati huo pia, Wenger alipendekeza kuwa Mesut Ozil na Alexis Sanchez wataendelea na mikataba yao huku mazungumzo ya mkataba mpya yakiendelea.


Comments
Post a Comment