ARSENE WENGER AFARIJIKA KWA MSHINDO WA TANO

Klabu Ya Arsenal Imefanikiwa Kupata Point 3 Kwa Kupata Ushindi Dhidi Ya Everton Siku Ya Jumapili


Mechi iyo iliyopigwa kwenye uwanja wa nyumbani kwa Everton, Goodison Park ilikua ya ushindani mkubwa ambapo timu ya arsenal ilionekana inashambulia kwa upande mkubwa kuliko Everton katika vipindi vyote viwili vya mchezo huo. Rooney ndiye alianza kuipachikia Everton bao la kwanza dakika ya 12 ya mchezo huo na goli ilo kudumu mpaka dakika ya 40 ambapo Monreal wa arsenal alirudisha goli hilo, kisha M Ozil (53),A Lacazette (74),A Ramsey (90) na A Sanchez (90+5) kuwamaliza kabisa Everton kwa kumalisha bao 5-2.


Kwa matokeo ayo arsenal inaikaribia top 4 kwa kuwa na alama 16 sawa na timu ya Chelsea ambapo Manchester City anaongoza ligi kwa alama 25.

Comments