MWANARIADHA WA UINGEREZA Mo Fa AMEFANIKIWA KUSHINDA MBIO ZA MITA 10,000...
Mo Farah usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kushinda mbio za mita 10,000 na kubeba medali ya dhahabu akitumia dakika 27:05.17 huku mkenya Paul Tanui akiwa wa pili na kubeba medali ya fedha
Farah,33, ameweza kutetea mbio hizo alizoshinda katika michuano ya Olympic London 2012, na sasa kuwa amekuwa ni mwanariadha wa kwanza wa Uingereza kuchukua medali 3 za dhahabu katika Olympic.
Medali hii inafanya Uingereza kufikisha medali 10 za dhahabu katika michuano hii ya Olympic mwaka huu.
kazi nzuri kutoka kwake
ReplyDelete