NI MUDA WETU TENA WA KUPATA HABARI 5 KALI BORA ZA WIKI NZIMA NDANI YA BLOG YAKO PENDWA YA BESTHANDSDAY

Ni Siku Yako Mdau Wa Besthandsday Blog Yako Bora Zaidi Tanzania Kupata Best News (B5N) Za Wiki Nzima
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjQ6MJ3rk3LLG5hbmFkCfWZHZXrMYmQdicPs5FKBkObJsa3ro6IVx0TuXsj00LOQ-87BoU7jA-26MMm3CYNfRbdxMT0_FlscV5bBpeRJLFM3_q7anzhYuK2OfmYeD7ubSpB5FtMWRTn3Hc/s1600/top-5-best-ios-features1-007.jpg

 BN#01 RAIS Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Amezindua Rasmi Ujenzi Wa Mradi Wa Barabara Ya Juu kwenye Makutano ya Ubungo (FlyOver ya Ubungo) Itakayoanza kujengwa Hivi Karibuni.

Akiuelezea mradi huo Rais Magufuli amesema Ujenzi wa barabara juu ya Ubungo utatumia miezi 30 kukamilika na utagharimu jumla ya TZS bilioni 188 ambapo bilioni 186 zinazotolewa na Benki ya Dunia (WB) na zingine zitatolewa na serikali ya Tanzania.
Aidha Fly-Over ya Ubungo itakuwa na (ghorofa) njia tatu, njia ya chini, ya kati na juu. Ambapo njia ya chini itakuwa ni ya Morogoro – Mjini Kati, Barabara ya juu itakuwa ni kwa ajili ya gari za Mwenge – Tabata huku njia ya kati itakuwa makutano kwa wanaohitaji kubadili njia.
Kwa upande wake, Rais wa Benki ya Dunia (WB), Dkt. Jim Kim ambao ni wafadhili wakuu wa mradi huo, wamejidhatiti kuendelea kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania

 BN#02 Samatta Aing'arisha Taifa Stars,Yanga,Azam Zatolewa Shirikisho,Yanga Yapangiwa Fc Alger

Jumamosi ya March 25 2017 uwanja wa Taifa Dar es Salaam nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta aliingia uwanjani kuiongoza Taifa Stars kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Botswana “Zebra” katika mchezo uliyopo katika kalenda ya FIFA

Huu ni mchezo ambao Taifa Stars ambayo ipo chini ya kocha wa muda Salum Mayanga baada ya kocha wa zamani Boniface Mkwasa kumaliza mkataba wake, ulikuwa ni muhimu hususani kuporomoka kwa Stars katika viwango vya FIFA kufikia hadi nafasi ya 157 wakati Botswana wao wakiwa nafasi ya 116.

Taifa Stars imefanikiwa kupata ushindin wa goli 2-0 magoli ya Taifa Stars yakifungwa na nahodha wao wa Mbwana Samatta dakika ya 2 na dakika ya 87 ya mchezo, Taifa Stars sasa itarudi tena uwanjani Jumanne ya March 28 kucheza dhidi ya Burundi katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam

BN#03. Waziri Nape Atumbuliwa Sekta Ya Uwaziri Wa Michezo Nafasi Yake Achukua Mwakyembe

 A.Avalia Njuga Swala la uvamizi wa mkuu wa mkoa Clouds

B.Anakwenda kituo cha clouds kujionea hali halisi

C.Anakutana na wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuzungumzia hatua atazochukua

D.Anaunda kamati ya kumchunguza mkuu wa mkoa

E.Kamati inatoa ripoti anakabidhiwa na kuwwambia waandishi ataipeleka kwa wakubwa zake yaani Waziri mkuu na Rais

F.Anatumbuliwa,anaitisha waandishi kuwaaga,anatolewa bastola.

G.Aitwa Shujaa kwa kusimamia Haki.

Rais John Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam imesema katika mabadiliko hayo, Rais Magufulia amemteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

  BN#04 Rais Magufuli Kuwapisha Mabalozi Wapya Na Mabalozi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 24 Machi, 2017 amewaapisha Mawaziri wawili, Katibu Mkuu Ikulu, Mabalozi wanne na Kamishna wa Tume ya Mahakama, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Walioapishwa ni Mhe. Dkt. Harrison George Mwakyembe aliyeapishwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi aliyeapishwa kuwa Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, na Bw. Alphayo Kidata aliyeapishwa kuwa Katibu Mkuu – Ikulu.
Wengine ni Mhe. Sylvester Mabumba aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Dkt. Abdallah Possi aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Job Masima aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Israel na Mhe. Jaji Stella Esther Mugasha aliyeapishwa kuwa Kamishna wa Tume ya Mahakama.
Akizungumza baada ya kuwaapisha viongozi hao, Mhe. Rais Magufuli amewataka kuchapa kazi kwa juhudi, maarifa na kwa kutanguliza maslai ya Taifa na pia amewasihi kutobabaishwa na kauli ama vitendo vyovyote vya kuwavunja moyo.
Mhe. Rais Magufuli pia amewasihi waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari kufanya kazi zao kwa weledi na kwa kutanguliza maslai ya Taifa badala ya kutoa kipaumbele katika masuala ya migogoro na mambo mengine yasiyo na manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
“Nchi yetu huko nje ina sifa kubwa sana, juzi tu hapa amekuja Rais wa Benki ya Dunia na amekubali kutupatia Shilingi Trilioni 1.74 na pia Benki ya Dunia ipo katika mchakato wa kutupatia fedha zingine Shilingi Trilioni 2.8 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, haya ndio mambo muhimu ya kuandika lakini hebu angalia siku iliyofuata jinsi magazeti yalivyoandika” amehoji Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, amewaonya wamiliki wa vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikiandika habari za uchochezi na amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe kuhakikisha vyombo vya habari vinafanya kazi kwa kufuata sheria na havitumiwi kuvuruga nchi.
Kabla ya kuwaapisha viongozi hao, Mhe. Rais Magufuli amepokea hati za utambulisho za Mabalozi 6 walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi hao ni Balozi wa Cyprus hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Muscat – Oman Mhe. Andreas Panayiotou, Balozi wa Bangladesh hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Nairobi – Kenya Mhe. Meja Jenerali Abdul Kalam Mohammad Humayun Kabir na Balozi wa Nepal hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Pretoria – Afrika Kusini Mhe. Amrit Bahaur Rai.
Wengine ni Balozi wa Ecuador hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Addis Ababa – Ethiopia, Balozi wa New Zealand hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Pretoria – Afrika Kusini na Balozi wa Jamhuri ya Kongo mwenye makazi yake Mjini Kigali – Rwanda Mhe. Michael Gerrard Burrel.
Katika mazungumzo yake na Mabalozi hao Mhe. Rais Magufuli amewapongeza kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na amewahakikishia kuwa Tanzania itaendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano na nchi hizo, huku akitilia mkazo ushirikiano katika masuala ya uwekezaji, biashara na kubadilishana uzoefu katika uzalishaji mali hususani kilimo.

BN#05  Muswada Wa Bima Ya Afya Wa Trump Wakataliwa


Rais wa Marekani Donald Trump amewalaumu wapinzani wake wa cham cha Democrats kwa kushindwa kuidhinishwa kwa mpango wake wa afya.
Mabunge yote mawili yanadhibitiwa na wanachama wa Republican lakini muswada huo uliondolewa siku ya Ijumaa kwa sababu ulishindwa kupata kura ulizohitaji.
Akizungumza na gazeti la washington Post, Trump alisema ''hatukuweza kupata kura hata moja kutoka kwa wanachama wa Democrat na tukaona haya hivyobasi kuondoa muswada huo''.
Kuondolewa kwa muswada huo katika dakika za mwisho ni pigo kubwa kwa rais.
Hatua ya kuuondoa muswada huo wa Obamacare ilikuwa mojawapo ya ahadi zake za uchaguzi wakati wa kampeni.
Spika wa bunge Paul Ryan alisema kwamba yeye na bwana Trump walikubaliana kuuondoa muswada huo ,baada ya kubainika hautapata kura 215 za chama cha Republican zilizohitajika.
Chama cha Republican kina wanachama wengi katika mabunge yote mawili ya uwakilishi na Seneti.
Hatahivyo, ripoti zilisema kwamba kati ya wanacha 28 hadi 35 wanapinga sheria hiyo mpya ya afya ya rais Donald Trump.
Wengine walidaiwa kutofurahishwa kwamba muswada huo ulikuwa unapunguza sana bima ya afya huku wengine wakidai kuwa mabadiliko hayo hayatoshi.
Muswada huo pia hakupendelewa na umma huku asilimia 17 pekee ukiuunga mkono.
Trump amesema kuwa amejifunza mengi kufuatia hatua yake ya kutaka kuuondoa muswada huo ikiwa ni miongoni mwa ahadi zake za kampeni ya uchaguzi alizotoa.
Amesema kuwa sasa ataangazia marekebisho ya kulipa kodi.
Kiongozi wa chama cha Democrat Nancy Pelosi amesema kuwa ni ushindi wa raia wa Marekani.
Trump alikiri kwamba mabadiliko ya bima hiyo ya afya yaliofanywa na mtangulizi wake Barrack Obama yatasalia kutekelezwa kufuatia kushindwa kwa chama cha Republican kuuondoa OBamacare.



Comments

Post a Comment