Siku Ya Jumapili 24.02 Ni Fainali Ya Carabao Cup Dhidi Ya Arsenal Na Manchester City Uwanja Wa Wembley
Ni mechi kali siku ya kesho ambapo timu kubwa za EPL zitapomenyana kuwania kombe la Carabao kwenye uwanja wa Wembley. Upande wa Arsenal unaongozwa na kocha mkongwe kuliko wote EPL Arsene Wenger na upande wa Manchester City kikosi kikinolewa na Master Plan Pep Guardiola.
Msimu uliopita kombe ilo lilibebwa na Manchester United, Je msimu huu nani atachukua kati ya Arsenal the gunners na Manchester City? Arsenal ikijivunia wachezaji wao wapya Mikhi na Aboumeyang wanayonafasi kubwa ya kupata ushindi siku iyo ya kesho, uku Manchester city wakijiamini na kurudi kwa hali nzuri ya mshambuliaji wao Kun Aguero, Kevin De Bryune na Rahim Sterling. Arsene Wenger aliweza kutoa kafala mechi ya Europa dhidi ya Ostersunds ili kukiweka sawa kikosi cha kwanza watachokipiga na Man city.
Comments
Post a Comment