RAISI MPYA WA AFRIKA KUSINI KUAPISHWA

Mwenyekiti Wa Chama Tawala ANC Nchini Afrika Kusini Bwana Cyril Ramphosa Aapishwa Kuwa Raisi 


Mwenyekiti wa chama tawala cha ANC Cyril Ramaphosa amepishwa kuwa rais wa Afrika Kusini baada ya rais wa taifa hilo Jacob Zuma kujiuzulu.

Rais huyo mpya alikuwa mtu wa pekee aliyeteuliwa siku ya Alhamisi huku uteuzi huo ukiungwa mkono kwa shangwe bungeni.

Bwana Zuma alikuwa chini ya shinikizo kali kutoka kwa chama chake cha ANC kilichomtaka ajiuzulu la sivyo akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani dhidi yake bungeni.



Katika taarifa ya runinga, alisema kuwa anajiuzulu mara moja lakini hakubaliani na uamuzi wa chama.

Bwana Zuma anakabiliwa na madai kadhaa ya ufisadi lakini amekana kufanya makosa yoyote.

Akiwa naibu wa rais Ramaphosa anakuwa kaimu wa rais mara moja baada ya Zuma kujiuzulu....Source @ bbcswahili.com


Sponsors Ads Call: 0759 85 02 59




Comments