KUELEKEA FAINALI UEFA RONALDO CR7 ATEMA CHECHE

Ronaldo Akataa Kufananishwa Na Salah Kiuchezaji Na Kupania Ushindi Dhidi Ya Liverpool


Mchezaji bora mara 5 duniani, Cristiano Ronaldo amesema hatakai kufananishwa na Salah ambaye amekua na msimu mzuri kwenye EPL kwa kuchukua kiatu cha mchezaji bora na michuano ya ulaya kwa kuisaidia timu ya Liverpool kufika fainali kwa sababu yeye ni mchezaji mrefu zaidi ya Salah, anatumia miguu yote na pia hutumia kichwa kupata magoli muda wowote na ivyo ametaka wapenzi wa mpira miguu kumfananisha Moamed Salah na Messi.


Fainali ya UEFA itachezwa siku ya Jumamosi tarehe 26 mwezi huu mji wa Kiev nchini Ukraine, ambapo Real Madrid ambao ni mabingwa mara 2 mfululizo itawania kombe ilo kwa mara ya tatu mfululizo uku Liverpool ikijitahidi kufuta mkosi kwa kuchukua kombe ilo toka walipochukua mara ya mwisho mwaka 2004. 

Comments