MIKE PENCE AITWA MJINGA NA KOREA KASKAZINI

Makamu Wa Raisi Wa Marekani Mike Pence Alaumiwa Kwa Kuitwa Mjinga Na Afisa Wa Cheo Cha Juu Nchini Korea Kaskazini 


Choe Son-hui alisema Pyongyang haitaweza kuibembeleza Marekani kwa mazungumzo.
Siku za hivi karibuni pande hizo mbili zimeonya kuwa mkutano wa Juni 12 unaweza kuharishwa au kufutwa kabisa.

Korea Kaskazini ilisema itafikiria tena iwapo itahudhuria mkutano ikiwa Marekani itaendelea kusisitiza kuwa iachane na mpango wa silaha za nyuklia.
Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumanne alisema Korea Kaskazini ndiyo ingetimiza masharti ya kufanyika kwa mazungumzo hayo.


Choe Son-hui amehusika kwenye mazungumzo mara kadha na Marekani kwa karibu miaka kumi iliyopita.
Alimuita Mike Pence mjinga kwa kuifananisha Korea Kaskazini, taifa la nyuklia na Libya, ambayo anasema ilikuwa na vifaa vichache tu ilivyokuwa ikicheza navyo.
"Kama mtu ambaye nimehusika kwenye masuala ya Marekani, siwezi kuficha mshangao wangu kufuatia matamshi kama hayo ya kijinga yanayotoka kinywani mwa Makamu wa Rais wa Marekani," alisema.
source @ bbcswahili.com

Comments