NCHI YA RWANDA KUDHAMINI KLABU YA ARSENAL

Rwanda Kushirikiana Na Klabu Ya Arsenal Ili Kukuza Utalii Nchini Mwake


Kwa mujibu wa mapatano hayo,Rwanda itakuwa mshirika rasmi wa Arsenal wa sekta ya utalii Kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia msimu ujao , fulana za timu ya Arsenal mkono wa kushoto zitakuwa na nembo yenye maneno ya 'visit Rwanda' au ''Tembelea Rwanda''.

Hii itahusu timu ya kwanza,timu ya wachezaji walio chini ya umri wa miaka 23 na timu za wanawake.Pia imetangazwa kwamba maneno hayo ya Tembelea Rwanda yatakuwa yakionekana kwenye mabango maalum ya kibiasara ndani ya uwanja wa Emerates wakati wa mechi za Arsenal.

Mkataba huo ulisainiwa Jumanne baina ya klabu ya Arsenal na mamlaka ya maenedeleo ya Rwanda kupitia kitengo chake kinachohusika na utalii na maendeleo

Haikutangazwa ni kitita kiasi gani cha pesa ambacho Rwanda imetoa ili kutangazwa kwenye jezi za Arsenal.

source@bbcswahili.com

Comments