SASA NI HABARI KAMILI: EMERY NDANI YA THE GUNNERS

Klabu Machachari Ya Arsenal Imkamilisha Saini Ya Kocha Wa Zamani Wa PSG Unai Emery


Baada ya sintofahamu iliyobujikwa kwa mashabiki wa arsenal ulimwenguni kote ya ni nani atachukua viatu vya mzee Arsene Wenger baada ya kustaafu mwishoni mwa msimu huu, bodi ya wakurugenzi imefanya uchaguzi na kuamua kupataia kocha wa zamani wa PSG na Sevilla bwana Unai Emery ili kushika mikoba ya mzee wenger aliyedumu na klabu io zaidi ya miaka 22.


Kocha mpya uyo ataihudumia klabu iyo ambayo imemaliza katika nafasi ya sita kwenye msimu huu ikikosa nafasi ya kushiriki ligi kuu ya mabingwa barani ulaya. Unai Emery ameweza kumpiku Arteta ambaye pia alikua anapewa nafasi ya kuchukua mikoba ya mzee Wenger licha ya Arteta mwenyewe kufurahia na kupongeza uchaguzi wa Emery kwani anaamini uzoefu wake utasababisha kuleta chachu ya mafanikio katika klabu iyo.

Comments