NANI ATAIBUKA MBABE WA AFCON 2021, SENEGAL AU EGYPT? MANE AU SALAH?

Imeandikwa na Mr. Peter John (PBD T) | Mdau wa Michezo nchini Tanzania

KAMA mpenzi wa mpira wa miguu unaweza kuungana na mimi katika furaha ya kushuhudia fainali kubwa kabisa la kombe la mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON 2021, linalofanyika nchini Cameroon mwaka huu 2022. Kombe hili lenye historia maradufu kwa wachezaji na wapenzi wa mpira nchi zote za Afrika na duniani kwa ujumla, lilikua lifanyike mwaka jana 2021 ila kutokana na changamoto za ugonjwa wa UVIKO 19 (COViD 19) lilisogezwa mbele na hatimaye limeweza kufanyika mwaka huu kuanzia tarehe 9 Januari na litamalizika tarehe 6 Februari nchini Cameroon.

FURAHA na bashasha kuu nliyonayo na mashabiki wengi wa mchezo huu pendwa ni kuona timu mbele kubwa zitapomenyana kuwania kombe hilo la AFCON 2021 katika uwanja wa Olembe Stadium uliopo Yaounde nchini Cameroon mida ya saa 4 usiku kwa majira ya Afrika Mashariki. Pongezi sana kwa nchi ambazo timu zao za taifa ziliweza kushiriki, pia pongezi kwa timu ya taifa ya Cameroon kwa kuwa mshindi wa 3 kwa kuifunga timu ya taifa Burkinafaso kwa ushindi wa mikwaju ya penalty 5-3 na ivyo kuweza kufuta machozi kwa kupoteza nafasi ya kushiriki mechi ya fainali. "Mcheza kwao hutunzwa" waswahili wasema, kwa ushindi nafasi ya 3 sio mbaya pongezi kwao.

KIVUTIO Kikubwa kwenye Fainali ni kuzikutanisha timu ya taifa SENEGAL (Simba wa Teranga) dhidi ya EGYPT, ambapo zina wachezaji wawili wakubwa katika ulimwengu wa mpira uku wakichezea klabu moja inayoshiriki ligi Kuu na pendwa ya EPL nchini Uingereza. Hapa nazungumzia SADIO MANE na MOHAMMED SALAH, wachezaji wa daraja la juu kabisa kwenye soka la Ulaya wakikipiga Liverpool fc wakiaminiwa na kocha Klopp katika safu ya ushambuliaji wa timu iyo na wakiwa chachu ya mafanikio ya Liverpool katika kushinda ubingwa wa UEFA mwaka 2018, Super cup na Ligi Kuu EPL msimu wa mwaka 2019/20.

Kwa SENEGAL (lions of Teranga) imefuzu kuingia hatua ya fainali kwa ushindi waliopata 3-1 dhidi ya Burkinafaso katika hatua ya nusu fainali. Mchezaji wao nyota Sadio Mane, amekua msaada mkubwa katika safu ya ushambuliaji kuanzia hatua ya makundi akihusika kwenye magoli ya ushindi karibia kila hatua. Mane amekua akitegemewa pia katika klabu yake ya Liverpool kama msanifu wa ramani za ushindi na amekua akihusika maradufu kwenye ushindi muhimu wakati wote kwenye makombe barani ulaya. Kuelekea fainali ya leo, Mane (10) jezi mgongoni naamini atapewa kitambaa cha unahodha uku mategemeo ya waSengali na mashabiki wengi wa mpira wakiwa na Imani kubwa kwake kuwezesha ushindi.


Na EGYPT (Mafarao wa Misri) imefanikiwa kufuzu kuingia fainali kwa kuwapiku wenyeji Cameroon kwa mikwaju ya penalty, kwenye mchezo mgumu na mkali wenye kusisimua wakiwaacha midomo wazi wenyeji kwa kile wasichokua wakitegemea. Salah (10) jezi mgongoni alipata goli kwa penalty baada ya dakika 120 za mchezo huo. Katika muda wote wa mchezo huo wa nusu fainali, Salah (10) hakuweza kuonyesha makeke na cheche zake zilizimwa na bwana mdogo kutoka beki ya Cameroon anayeitwa Tolo. Nyota wa Misiri, Salaha (10) ni mchezaji hatari sana kwa kufumania nyavu mara kwa mara akiwa Liverpool na ni mmoja wa wafungaji wakuogofya barani ulaya na ligi kuu EPL. Mashabiki na wapenzi wa mpira watakua na Imani kubwa kwake katika kufanikisha ushindi na kunyanyua kombe la AFCON 2021.

Ni TUKIO la kihistoria katika nyakati hizi za mpira barani Afrika, kwa timu za taifa zilizofika faniali AFCON 2021 “SENEGAL (Lions of Teranga) vs EGYPT” Zikiwa na wachezaji wakubwa wawili uku kila timu ikiwa na wake wanaochezea klabu moja kubwa barani ulaya “Liverpool fc” uku wakiwa tegemeo kubwa na sasa wanakuatana katika pande tofauti za mataifa wakiwa kwenye nafasi ya kubeba mataifa yao siku ya Fainali na kushinda kombe. Nafikiri kwa sauti ndogo, Salah na Mane wangekua na uwezo wangeomba lile kombe ligawanywe vipande viwili na ziweze kupewa timu zao za taifa kila mmoja aweze kufurahi. Kwa uzito wa mchezo huo wa fainali, ni kitu ambacho hakiwezekani ivyo inabidi apatikane mshindi mmoja ambapo upande wa Egypt (Mafarao wa Msiri) watakua wakimuangalia zaidi SALAH (10) na Senegal (Simba wa Teranga) watakua wakimtegemea zaidi MANE (10) kwenye kuafanikisha ubingwa.


UTABIRI wangu katika mechi ya fainali AFCON 2021 zinazowakutanisha SENEGAL vs EGYPT, kwanza nikuangalia mchezo wenye nidhamu kubwa sana kutokana na aina za wachezaji wa kimataifa kutoka timu zote mbili. Pia, Senegal ni timu inayocheza kuishindi ata ukiangalia njia yao kufika hatua ya fainali sio ya kusua sua. Wamekua wakicheza kama mabingwa uku wakijiamini, kujitambua na wamekua na uwezo wa kubadilika kutokana na mchezo unavyokwenda dhidi ya wapinzani wao muda wote.


Nikiwatupia jicho la tatu Misri, wamekua watu wakuwashangaza wapinzani kwa kuwapa matokeo wasioyategemea muda wote wa kombe hili la AFCON 2021. Egypt wameanza kwa udhaifu uku wakiwa wanaimairika kila mechi kuanzia hatua ya makundi na kuweza kuitoa Cameroon ambapo mashabiki wengi wa mpira hawakutegemea kama mafarao wa Misri wataweza kufika fainali katika kombe hili. Salah (10) amekua na kiwango sio cha kutisha kama ilivyotegemewa, ila kinachoibeba Misri ni kila mchezaji kuwa na hari ya utayari, kujituma na kujipa moyo wa ushindi.

KARATA yangu naitupa kwa Senegal (Simba wa Teranga) kupata ushindi ndani ya dakika 90. Naamini Mane (10) ataweza kuthibitisha ubora wake wa Liverpool kwa timu yake ya taifa na mashabiki wote wa mpira wa miguu duniani. Pia kikosi chake kipo kwenye hali nzuri sana wakiwa na wachezaji wakali kama beki yao hatari Koulibaly (3) anayecheza klabu ya Napoli inayoshiriki ligi kuu Italia na kipa Edouard Mendy (16) anayecheza Chelsea fc.

JAPO yote yanawezekana kwenye mpira wa miguu, ivyo tutegemee mchezo safi kabisa kutoka kwenye fainali hii ya AFCON 2021 itayochezwa pale nchini Cameroon uwanja wa Olembe, pia tutegemee kuwaona nyota wa klabu kubwa nchini ulaya Mane (10) na Salah (10) wakipambania timu zao za taifa kwenye kufanikisha ubingwa. Ikumbukwe pia, Misri ndio inaongoza kwa kuchukua kombe hilo mara nyingi kuliko timu yoyote ya Afrika mara 7, uku Senegal (Lions of Teranga) wakiwa hawajawahi kuwa mabingwa ata mara moja ila wakiingia hatua ya fainali mara nyingi na kuishia nafasi ya 2.

KIKOSI XI upande wa Senegali (Simba wa Teranga) kinachotegemewa kuanza usiku wa leo; Mendy, Sarr, Koulibaly, Diallo, Ciss, Gueye, Mendy, Gueye, Dia, Diedhiou, Mane

KIKOSI XI upande wa Eypt (Mafarao wa Misri) kinachotegemewa kuanza usiku wa leo; Gabal; Ashour, Abdelmonem, Wensh, Fotouh; Sherif, Elneny, Fathy; Marmoush, Salah, Mohamed.

Ni matumaini yangu hutwaweza kukosa kuangalia mtanange huu kupitia luninga au simu janja kwa kupata matangazo ya moja kwa moja kutoka Cameroon. Makala hii itapatikana pia kupitia mtandao wa https://thisisrealpeterjohninafrica.blogspot.com/ . Kwa mawasiliano zaidi whatsapp me: +255 759 580 259 ! 

 

Comments